Thursday, 12 July 2012

VIJANA WA KINA LAUWO KUJIFUNZE KWA BABU ZETU

ningependa kuwafahamisha kuwa ningependa kufufua umoja wa  wanalauwo waishio ndani na nnje ya tanzania , nia na madhumuni ni kuwaleta pamoja wana lauwo wote, huu ni mtazamo ambao ulianzishwa na babu zetu enzi hizo lakini kwa kipindi chao ilikuwa ngumu kwani mawasiliano hayakuwa  ya kisasa kama sasa. Labda kwa kumbukumbu niwakumbushe vijana wenzangu wakina lauwo kuwa kuna  Mchungaji  JACKOB LAUWO ambaye sasa ni marehemu, Christophoro lauwo marehemu na wengi, Epafra Lauwo, apeli lauwo, Biliam lauwo, na wengi nilio wasahau enzi nikiwa na umri wa miaka kama kumi na moja, walijitahidi kufanya vikao vya kuleta ukoo wetu pamoja lakini ikashindikana kwani mawasiliano hayakuwa mazuri kama sasa, Cha kufanya ni bora sisi tunaokuwa kuwa na umoja wetu wa vijana wa kinalauwo ndio utakao tupa mwelekeo wa kujuana kwa ukaribu zaidi. kwenye face book nilitoa namba yangu yasimu, na nimeanja kupokea simu kwa vijana wenzangu wa kinalauwo. Nina idadi ya watu kumi sasa waishio dar es salaam. Asanteni