Monday 23 July 2012

mtazamo wangu kuhusu kukutana kwenye ubarikio

Ni jambo la kusara na la heri kukutana wakati wa sikukuu kwani ndugu jamaa huletwa karibu wakati wa furaha na inakuwa ni rahisi  kujuana na kukumbukana kwa matukio ya sikukuu hizo.
      Je? isingekuwa jambo la muhimu kukakutana kwa makundi ili ifikapo december ikawa nirahisi kujumuika kwa pamoja nikiwa na maana hii, makundi ; namaanisha kutoka mikoa mbali mbali kwa mfano kwa walioko
Dar es salaam  kundi la  1
Arusha  kundi la 2
Mwanza  kundi la  3 
Mbeya  kundi la 4
 Kilimanjaro kundi la  5
Manyara  kundi la  6 
Singida  kundi la 7
Dodomakundi la  8
Morogoro la 9, na kuendelea kwa walioko ndani ya nchi ya tanzania lakini kwa walioko nje ya nchi hatutawasahau kwani tutawapa kundi  maalumu nikiwa  na maana kuwa ni vigumu kutaja nchi zote wanapoishi,
      Ila makundi haya yatakuwa na kiongozi mmoja ambaye atakuwa anawafahamu japo kwa majina na namba za simu waliopo kwenye kundi lake, ili ifikapo mwezi wa dec ( kuhiji ) basi iwe rahisi kupeana taarifa nani kafika na nani hajafika,

Umuhimu wa makundi haya:
1. Kukiwa na jambo kama harusi ni rahisi kupeana taarifa.
     namaanisha kuwa kuna dada zetu wanaolewa inapofika zamu ya kaka, inakuwa aibu,
     kwa upande mwingine ni kwetu sisi. Kwa mpango huu inakuwa raisi kuchagiana angalau kidogo              kulingana na uwezo wa  alicho nacho mtu mfukoni na kikaonekana kikubwa kwani ni cha pamoja.

2. wakati wa matatizo nirahisi kumfikishia kiongozi wako, wa kundi la mkoa uliopo na akawafikishia wengine taarifa si mpaka juje kusikia kwa mtu back

3. Taarifa za kazi , japokuwa wengi hawapendi ila mimi nasema, (niseme!!!!!!!)
hatakama itakuwa ngumu basi mfikishie taarifa mtu apigane mwenyewe kwenye mchakato wa interview

4.  naomba nimalizie kesho  faida hizi na  mwenye  faida na mchango kama huu au kinyume basi nenda sehemu ya comment uweke. ili tuweze kujumuika kwa upamoja kama   .........................................